WATUMISHI WAPYA WAASWA KUZINGATIA MAADILI

Imewekwa: 09 Jan, 2025
WATUMISHI WAPYA WAASWA KUZINGATIA MAADILI


Na Mwandishi Wetu,
 Morogoro.

Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Mhe. Usekelege Mpulla,amewataka watumishi wapya kuzingatia misingi ya maadili ya Utumishi wa Umma, ikiwa ni pamoja na kuwa wa mfano.

Ametoa wito huo leo Januari 8, 2025 wakati akifunga mafunzo  elekezi ya awali kwa watumishi wapya wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mkoani Morogoro.

Aidha, amewataka watumishi hao kuwa Mabalozi wa taasisi katika vituo vyao vya kazi kwa kufanya kazi kwa bidii huku wakizingatia Sheria na taratibu za utumishi wa Umma.


Vilevile, ametoa pongezi kwa kitengo cha utawala kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwashukuru wahadhiri na wawezeshaji kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, tawi la Mbeya kwa kuwezesha kuwapatia ufahamu, na uelewa wa utumishi wa umma  watumishi hao wapya kwa ajili ya ustawi wa taasisi na Taifa kwa ujumla.

Sambamba na hayo, amewataka watumishi hao kuwa waaminifu na kutumika kwa maslahi ya umma  kwa kufanya kwa vitendo yale waliyo jifunza.