Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Fomu ya rufaa iliyojazwa ni lazima ikabidhiwe kwa upande mwingine. Unaweza kufanya hivyo kwa mojawapo ya njia zifuatazo:-
Kabidhi nakala ya fomu kwa upande mwingine
Nukushi fomu kwa upande mwingine
Tuma nakala ya fomu upande mwingine kwa njia ya rejesta ya posta.
Kujaza fomu CMA F.1
Kuleta mgogoro mbele ya Tume ndani ya siku 30 baada ya kuachishwa kazi. Iwapo siku 30 zimepita maombi ya kusikilizwa nje ya muda yanaletwa mbele ya Tume kwa kujaza fomu CMA F.2, taarifa ya maombi na hati ya kiapo.
Kujaza fomu CMA F.1
Kuleta mgogoro mbele ya Tume ndani ya siku 60 baada ya mgogoro kutokea. Iwapo siku 60 zimepita maombi ya kusikilizwa nje ya muda yanaletwa mbele ya Tume kwa kujaza fomu CMA F.2, taarifa ya maombi na hati ya kiapo.
Wakati wa kufungua rufaa kwenye Tume ni lazima kuambatanisha uthibitisho wa kukabidhi fomu kwa upande mwingine.
Habari Mpya