MKURUGENZI MPULLA AWATAKA VIJANA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO MAHALI PA KAZI

Imewekwa: 29 Apr, 2025
MKURUGENZI MPULLA AWATAKA VIJANA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO MAHALI PA KAZI

Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Mhe. Usekelege Mpulla, ametoa wito kwa Wafanyakazi Vijana wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) kutokuwa chanzo cha migogoro mahali pa kazi  ili kuleta tija na ufanisi kazini.

Wito huo ameutoa wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi Vijana wa TUICO iliyofanyika  Aprili 26, 2025 Mkoani Singida.

Aidha amewasisitiza kuwa weledi na kuhakikisha mahali pa kazi panakuwa na amani, ili kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa Taifa lao.

“Vijana wengi mkijihusisha kwenye migogoro, mtapoteza muda mwingi kufuatilia kesi, uzalishaji utadorora na uchumi wa nchi utashuka”

Vile vile ameushukuru Uongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Kwa ushirikiano mzuri wanaotoa kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), kwa kutambua umuhimu na mchango wa wafanyakazi kwenye ustawi wa haki kazi na kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

Naye Mwemnyekiti wa TUICO Taifa Paul Sangeze, amemshukuru Mkurugenzi wa CMA kwa ushirikiano wake na vyama vya wafanyakazi na kumpongeza  kwa kuweka Mfumo mpya wa Usimamizi usajili wa Migogoro ya Kikazi (OCMS) ambao utachangia kupunguza kwa gharama za kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kushughulikiwa migogoro yao.