Mhe. Usekelege Mpulla

Usekelege Mpulla photo
Mhe. Usekelege Mpulla
Mkurugenzi Mkuu

Barua pepe: dir@cma.go.tz

Simu: 2136524 / 2136490

Wasifu

Kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), ninayo furaha kuwakaribisha kwenye Tovuti yetu mpya ambayo imeboreshwa na kutengenezwa kwa umahiri mkubwa kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu shughuli zinazofanywa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi hususani katika juhudi za kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.

Ni imani yangu kuwa tovuti hii itakuwa ni nyenzo sahihi itakazoiwezesha jamii kupata habari pamoja na elimu kupitia nyaraka mbalimbali. Aidha, tovuti hii ina video mbalimbali kwa ajili ya umma na hivyo kuifanya kuwa ni miongoni mwa sehemu muhimu za marejeo katika masuala mbalimbali ya utekelezaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha Sheria ya Taasisi za Kazi Sura Na.300 ya mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa mapipitio mwaka 2019 na imepewa jukumu la kutatua migogoro ya kikazi baina ya Mwajiri na Mwajiriwa.

Aidha, napenda kutaja mchango mkubwa na muhimu unaotokana na juhudi endelevu na itikadi yetu katika ubunifu na uboreshaji wa jitahada mbalimbali za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi inayokidhi viwango vya hali ya juu vya kiutendaji vinavyoifanya Tume kuwa taasisi ya mfano inayofanya shughuli zake za kila siku kwa kasi na ari inayokubalika. Jitihada hizi na nyingine ni matokeo ya uadilifu mkubwa wa menejimenti na watumishi waliodhamiria kuweka juhudi kubwa katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji huduma bora kwa umma.

Mwisho, lakini si kwa umuhimu, natoa wito kwa wadau wote kuendelea Kuvinjari Tovuti hii mara kwa mara na kuwasihi kuwasiliana nasi kwa na maoni, ushauri kwa ajili ya uboreshaji au kuhitaji ufafanuzi zaidi juu ya huduma zetu.

Tunawakushukuru kwa kuendelea kutuunga mkono na pia bado tuna ari kubwa ya kuendelea kushirikiana nanyi kwa ukaribu zaidi.

Mhe. Usekelege Mpulla

Mkurugenzi Mkuu