CMA YAENDELEA KUTOA DARASA LA UTATUZI WA MIGOGORO YA KIKAZI WIKI YA SHERIA.

Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) imeendelea kutoa elimu kwa Wananchi wanaojitokeza kutembelea mabanda katika maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere square jijini Dodoma.
Maonesho haya yanaambatana na utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali yanayotembelea katika maonesho , wakiwemo wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa utoaji elimu kwa moja ya makundi yaliyotembelea maonesho hayo Msuluhishi Mwandamizi kutoka CMA, Mhe. Thomas Malekela, amesema Tume ni chombo mahususi Cha kutatua migogoro ya Kikazi baina ya mwajiri na mwajiriwa.
Naye Msuluhishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Mhe. Belinda Kamoleka, ameeleza namna ya kusajili mgogoro mbele ya Tume, kwa njia ya mfumo mpya wa kusajili migogoro ya kikazi unaotarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni.

