JAJI MASABO AIPONGEZA CMA USIMIKAJI MFUMO WA KUSAJILI MASHAURI KIDIGITALI

Imewekwa: 13 Nov, 2024
JAJI MASABO AIPONGEZA CMA USIMIKAJI MFUMO WA KUSAJILI MASHAURI KIDIGITALI

Na Mwandishi Wetu,

Dodoma.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Dr. Juliana Masabo, ameipongeza Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Kwa kuanzisha Mfumo mpya wa kusajili Migogoro ya Kikazi Kwa njia ya mtandao unaofahamika kama ‘Online Case Management’ (OCMS).

Ametoa pongezi hizo wakati akimuapisha Msuluhishi wa CMA Mhe. Belinda Kamoleka, Mahakamani hapo leo Novemba 13, 2024, Jijini Dodoma.

Aidha Jaji Masabo amesema mfumo huo utarahisisha usikilizaji wa migogoro kwa wakati huku akiipongeza Tume kwa kufanikisha kuwa na mfumo unaosomana na Mahakama.

Aidha amemtaka Mhe. Belinda kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kutenda haki.