MHEDE AITAKA CMA KUONGEZA KASI USIKILIZAJI MASHAURI

Imewekwa: 03 Jul, 2024
MHEDE AITAKA CMA KUONGEZA KASI USIKILIZAJI MASHAURI

Naibu Katibu mkuu wizara ya mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Dk. Edwin Mhede amaeitaka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), kuongeza kasi katika usikilizaji mashauri Pamoja na kuongeza ufanisi ili maamuzi nanayofanywa yaweze kuwa bora.

Wito huu ameutoa alipotembelea banda la Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika maonesho ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam,tarehe 2Julai,2024.