MIZENGO PINDA ATOA WITO CMA KUONGEZA ELIMU YA UTATUZI WA MIGOGORO YA KAZI

Imewekwa: 08 Aug, 2025
MIZENGO PINDA ATOA WITO CMA KUONGEZA ELIMU YA UTATUZI WA MIGOGORO YA KAZI

Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda, ametoa wito kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kuongeza jitihada katika kutoa elimu kwa wadau kuhusu utatuzi wa migogoro ya kikazi, ili kuimarisha mahusiano bora mahala pa  kazi.

Mhe. Pinda ametoa  wito huo  Agosti 7, 2025, alipotembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake, katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo, Mhe. Pinda alipata fursa ya kutembelea na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.


 Kauli  mbiu ya mwaka huu ya  Maonesho hayo ni:
“Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.”