Mkurugenzi CMA, Ameahidi kushirikiana na Vyama vya Wafanyakazi Kikamilifu.

Imewekwa: 21 Mar, 2024
Mkurugenzi CMA, Ameahidi kushirikiana na Vyama vya Wafanyakazi Kikamilifu.

Mkurugenzi wa Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA), Mheshimiwa Usekelege Nahshon Mpulla, amesema Tume itaendelea kutoa ushirikiano Pamoja na kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kwani ndio mahala sahihi ambapo wafanyakazi wanapatikana na jukumu mojawapo kla Tume.
Ameyasema hayo leo Machi 15,2024 wakati akizungumza na kumkaribisha katibu wa (TUGHE) katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kinachofanyika jijini Dodoma.