Dira
Kuwa Tume ya mfano katika utatuzi wa migogoro ya kikazi Afrika Mashariki.
Dhima
Kuhimiza mazingira ya amani eneo la kazi kupitia usuluhishi na uamuzi kuimarisha uzalishaji nchini.
Lengo
Lengo kuu la Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ni kujenga ,kuimarisha na kukuza mahusiano bora na haki miongoni mwa waajiri na wafanyakazi Tanzania.
Tunu za msingi
Katika utekelezaji wa majukumu yake Tume itaongozwa na tunu za msingi zifutatazo:-
Uadilifu
Watumishi wetu watatekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kwa haki bila kutoa au kupokea rushwa ya aina yoyote katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yao. Hawatatumia rasilimali za uma kwa manufaa binafsi.
Utaalamu
Watumishi wetu watazingatia utendaji bora katika maadili ya kitaalam.
Utendaji wa pamoja
Watumishi watazingatia utendaji wa pamoja ili kuhakikisha utoaji bora wa huduma. Kutakuwa na mawasiliano ya nyanja zote ya uhakika.
Uwajibikaji
Watumishi watawajibika kwa matendo yao katika utekelezaji wa majukumu ya Tume.
Uungwana na Utu
Watumishi watawahudumia wateja na wadau kwa uungwana , utu na heshima kwa msingi wa kujiheshimu na kuheshimu wengine
Huduma kwa wateja
Watumishi watatoa huduma kwa usawa na kwa wakati. Huduma itatolewa kwa uwazi kwa wateja wote.