Usuluhishi

Usuluhishi ni mchakato ambao msuluhishi anakutana kwa pamoja au upande mmoja mmoja na wadaawa wenye mgogoro na kuangalia namna ya kuwasaidia wafikie makubaliano. Ni mchakato wa siri na husaidia pande kufikia mwafaka kwa haraka. Wakati wa mchakato huo pande zinaweza kupeana taarifa na kushauri namna ya kutatua mgogoro wenyewe. Msuluhishi anaweza kupendekeza namna ya kufikia suluhu. Makubaliano yanayofikiwa yanabana wadaawa na yanaweza kukaziwa kama tuzo katika Mahakama ya Kazi.

Migogoro ya kikazi inayowasilishwa kwa usuluhishi ipo ya aina mbilli yaani mgogoro wa haki na mgogoro wa maslahi. Kisheria mgogoro wowote lazima upitie hatua ya usuluhishi kabla ya kwenda hatua ya uamuzi, Mahakama ya Kazi, mgomo au wafanyakazi kufungiwa nje.

Mgogoro wa haki ni mgogoro unaohusu uvunjifu wa haki za kisheria, mkataba wa hali bora, au mkataba binafsi wa kiajira. Iwapo mgogoro wa haki utashindwa kupata suluhu mdaawa anaweza kupelekamgogoro hatua ya uamuzi au Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kutegemea aina ya mgogoro.

Mgogoro wa maslahi ni mgogoro unaotokana na utofauti wa tathmini juu ya jambo la kikazi la baadayeambalo halijawa haki na liko nje ya mkataba au sheria nahutokea pale makubaliano ya majadaliano ya pamoja yanaposhindikana. Iwapo usuluhishi utashindikana mdaawa anaweza kugoma au kufungiwa nje.

Iwapo upande uliokata rufaa utashindwa kufika kwenye usuluhishi mgogoro utatupiliwa mbali na pale ambapo upande mwingine utashindwa kufika mgogoro utaamuliwa upande mmoja

Usuluhishi