Uamuzi

Ni mchakato ambao mtu huru anateuliwa kama muamuzi ili kutatua mgogoro kwa kutoa uamuzi kuhusu mgogoro baina ya wadaawa.

Mgogoro wa kuamuliwa unahusu malalamiko juu ya:- ukomo wa ajira usio halali; uvunjifu wowote wa sheria ya kazi/kuvunja mkataba; sheria ya madhila; makosa ya madhila; uwajibikaji wa mwajiri kwa makosa ya mwajiriwa na mgogoro wowote unaoletwa kwa uamuzi na Mahakama ya Kazi.

Mgogoro wa maslahi iwapo wadaawa kwenye mgogoro wanatokea kwenye sekta ya huduma muhimu.

Mdaawa anaweza kuwakilishwa na mwanachama/afisa wa chama cha wafanyakazi au chama cha waajiri au wakili au mwakilishi binafsi.

Iwapo upande uliokata rufaa utashindwa kuhudhuria mchakato wa uamuzi, lalamiko linaweza kutupiliwa mbali. Iwapo wa upande mwingine utashindwa kufika mgogoro utaamuliwa upande mmoja.

Katika mchakato wa uamuzi kila upande utatoa ushahidi wa shauri. Kwa kuzingatia ushahidi na hoja za majumuisho za pande zote, muamuzi ataamua mgogoro kwa kutoa tuzo. Tuzo itatolewa kwa maandishi na inabana pande zote bila haki ya rufaa. Asiye ridhika na uamuzi huo anaweza kuomba marejeo Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi

Uamuzi unaweza kukaziwa kama tuzo ya Mahakama.

 

Uamuzi