Karibu

Habari!

Karibu katika tovuti mpya ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Katika jitihada za kufanikisha dira yetu ya kuwa Tume ya mfano katika utatuzi wa migogoro ya kikazi Afrika Mashariki, kuhimiza mazingira ya amani eneo la kazi kupitia usuluhishi na uamuzi, na kuimarisha uzalishaji nchini.

Lengo kuu la Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ni kujenga,kuimarisha na kukuza mahusiano bora na haki miongoni mwa waajiri na wafanyakazi Tanzania, ikitumia usuluhishi na uamuzi katika kutatua migogoro.

CMA, imedhamiria kudumisha amani kwa kushirikiana na vyama vya wafanyakazi serikali na mashirika binafsi ili kuweza kuleta, amani mahala pa kazi na kusaidia ongezeko la nafasi za ajira kwa kuzingatia wawekezaji kutoka nje ya Tanzania pamoja na ndani ya nchi kwa kuhakikisha tunatatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ili kuleta amani na kuokoa muda kwaajili ya uzalishaji bila kuadhiri uhuru wetu.

Usuluhishi wa migogoro mahala pa kazi ni chachu muhimu katika maendeleo ya sekta ya uwekezaji na fursa ya kutengeneza nafasi nyingi za ajira kwa vijana na watanzania nchini, kwani tunasuluhisha migogoro baina ya mwajiri na mwajiriwa Pamoja na mwajiriwa na mwajiri hivyo tunatengeneza amani na mshikamano imara mahala pa kazi kwa kuzingatia upatanishi baina ya wawekezaji na wazawa hii inatusaidia kukuza uaminifu na kukuza uwekezaji.

CMA, inaendelea kushirikiana na vyama vya wafanyakazi na waajiri pamoja na mashirika binanfsi ya ummma ili kuendelea kuwafgikia wafanyakazi na kutatua migogoro yao kwa haraka ili kuweza kuendelea na uzalishaji kwa lengo la kuimarisha na kukuza uchumi wa nchi na watanzania.

Aidha, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), inasaidia kutoa elimu kuhusu migogoro ya kikazi ikiwa ni pamoja na jukumu la kujitangaza ili umma uweze kuitambua vyema Tume.

Mwisho, CMA inaendelea na usuluhishi na uamuzi wa migogoro, hivyo ni wito wetu kwa watu wote wanaopitia changamoto mahala pa kazi kuja Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ili kuweza kupatiwa ufumbuzi, kwani ndio taasisis pekee inayotatua migogoro ya waajiriwa na waaajiri, na kutetea maslahi yao, kwani ndio madaktari bingwa wa migogoro ya kikazi na waleta tumaini jipya mahala pa kazi. Karibu tujenge uhusiano mwema kazini.