Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Brigedia Jenerali Hosea Ndagala (wa kwanza kulia), akiwa pamoja na Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi (wa pili kushoto), wametembelea banda la Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), katika Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake, katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo, yaliyoanza tarehe 28 Juni 2025 na yanayotarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai 2025, yanaongozwa na kaulimbiu: “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania.”